Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepata malalamiko kutoka kwa
watumiaji wa simu za mkononi kwamba kuna ujumbe unaosambazwa kwamba
ukipokea simu utapata madhara.
Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuwahakikishia wananchi kwa ujum;a
kwamba taarifa zinazoenezwa ni za uzushi na sio za kweli. Wananchi wanaombwa
kupuuza uzushi huo kwa kua hauna ukweli wowote.
Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuna tafiti nyingi zimefanyika
sehemu nyingi duniani, ambazo zimeonyesha kwamba kiwango cha mawimbi ya
mawasiliano hakina madhara kwa afya ya binadamu. Mamlaka inashauri watumiaji
wa huduma na wananchi wote kwa ujumla, kuendelea kuwa na imani na teknolojia
mpya zikiwemo za mawasiliano ya simu, utangazaji na utumiaji wa kompyuta,
ambazo hutumiwa ulimwenguni kote bila kuleta madhara yoyote.
Madhumuni ya Mamlaka ya Mawasiliano na watoa huduma za mawasiliano
kwa ujumla ni kuwaletea wananchi wa Tanzania mawasiliano bora kwa
kujenga miundombinu, kutoa huduma bora na matumizi mema.
Uzushi unaoenea upuuzwe kwa kuwa hauna ukweli wowote.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
No comments:
Post a Comment