Friday, July 9, 2010

LeBron James a.k.a King James aikacha Timu yake ya Nyumbani.

Mchezaji nyota wa mpira wa kikapu huko Marekani katika ligi maarufu ijulikanayo kama NBA Lebron James jana jioni ametangaza kuwa anaihama timu yake ya nyumbani Clevelenda Cavaliers na kuhamia timu ya Miami Heat. Ni matumaini ya LeBron ambaye anajulikana kama 'King James' kuwa akiwa Miami Heat atafanikiwa kutwaa ubingwa wa NBA kwa msimu unaokuja. Kwa sasa Miami Heat inaweza ikawa tishio katika ligi hiyo kwani LeBron sasa ataungana na nyota wengine wanaochezea timu hiyo kama Dwyane Wade na Chris Bosh ambao wote kwa pamoja na King James waliiwezesha timu ya Mpira wa Kikapu ya marekani kunyakua taji la Olympic miaka minne iliyopita huko Beijing.
Kwa Miami Heat sasa ni vicheko lakini kwa Clevelenda ni vilio na majonzi yaliyochanganyika na hasira za mashabiki wake iliyofanya baadhi ya mashabiki hao kuchoma jezi namba 23 ya nyota huyo.

NBA fans in Cleveland, Ohio, burn a LeBron James T-shirt  after learning of his decision to play for Miami.
Jezi ya King James ikipigwa kibiriti na waliokuwa mashabiki wake.

Nyota Dwyane Wade akipiga makofi wakati LeBron akitangaza uamuzi wake wa kuhamia Miami Heat hapo jana katika kipindi maalum kiitwacho 'The Decision' kinachotayarishwa na TV inayojihusisha na masuala ya michezo ESPN.

Kwa habari zaidi gonga hapa.

No comments:

Post a Comment