WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto , Bi. Magreth Sitta jana alikamatwa na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) baada ya kutuhumiwa kutaka kuwahonga wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanawake mkoani (UWT) Tabora ili wampatie kura.
Bi Sitta alikamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya Camise, iliyopo katika Mtaa wa Cheyo mjini hapa, ambapo alidaiwa kukutwa na pesa taslimu sh. milioni moja, simu saba za mkononi aina ya Nokia na akiwa na mipango ya kuzungumza na wajumbe wa mkutano huo kutoka katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora.
Kaimu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tabora, Bw. Bruno Rwenyagira ilisema Bi. Sitta alikamatwa saa tisa usiku akiwa katika mchakato huo.
Bw. Brona alisema kwamba majira ya saa 7.30 usiku walianza kutembelea nyumba za wageni ambazo wajumbe walishukia walipokua katika nyumba ya kulala wageni ya Maridadi waliona gari aina ya TOYOTA SURF yenye namba T 339 ANL ikisimama na wajumbe walioshukia katika nyumba hiyo walitoka na kumlaki Bi Sitta .
Baadaye alianza kuzungumza na Bw. Michael Manyanda na Bw. Abdu Musa na alipoona mahali hapo si salama aliondoka katika mazingira ya kutanisha ndipo maafisa hao walipoamua kuwakamata wapiga debe wake na kuanza upekuzi katika gest hiyo .
Bw.Julius Kilimanjaro ambaye ni Katibu wa Vijana Wilaya uyui akiwa katika ofisi ya TAKUKURU alipigiwa simu Bi. Sitta akimweleza kwamba anataka kuonana na mjumbe aliyeitwa Mama Nely.
TAKUKURU waliamfuata Mama Nelly aliyekuwa akihitajika na Bi. Sitta katika gesti ya Camise na kumkuta na mwenzake kisha kuchukuliwa hadi ofisi ya TAKUKURU kwa mahojiano zaidi .
Bi. Sitta alifika katika geti hiyo saa 7.55 usiku akiwa kwenye gari yake aina ya TOYOTA Surf yenye namba za usajili T 339 ANL na kuwekwa chini ya ulinzi na baada ya kupekuliawa alikutwa na sh 1,015,000,simu saba aina ya Nokia na bahasha za khaki 145 tupu.
Taarifa hiyo ya TAKUKURU inaeleza kwamba wiki iliyopita Bi. Sitta alikamatwa katika Wilaya Nzega akigawa vitenge na kanga na aliachiwa kwa dhamana.
Wengine waliokamatwa na Bi. Sitta ni Bw.Julius kilimanjaro Katibu wa Vijana Wilaya ya Uyui , Bi. Lucy Samueli Simwanza, Katibu wa Vijana Kata ya Ipuli, Bi. Elizabeth Kondolo, Katibu UWT Kata ya Lutende, Bi. Catheri Sepetu Mwenyekiti wa Kata ya Lutende Bw. Michael Manyanda Mkuu wa Green Gurd wa CCM Tabora na Mara joseph Mwalimu Shule ya Msingi Majengo Tabora.
Wengine wanaoshikiliwa ni Cosmas Urio dereva wa surf Rashid Abdala katibu mwenezi manispaa ya Tabora na Abdu Kayamba pamoja na vijana kadhaa wa umoja wa vijana wa CCM waliokuwa wameambatana na Waziri katika harakati hizo